The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mwijaku: Harmonize Piga Kazi, Kuhusu H-Baba……

0

MTANGAZAJI wa Clouds Media, Burton Mwenda maarufu kwa jina la Mwijaku ameamua kuvunja ukimya kufuatia H-Baba kumgeuka Harmonize na kuanza kumposti na kumsifia Diamond ilihali hapo awali alikuwa team Konde na alikuwa akimponda Diamond.

 

Mwijaku amemtaka Harmonize kujikita katika kazi yake na kuachana na mambo yanayoendelea mitandaoni huku akisema ni Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kutoa kasoro kwa kiumbe chake.

 

“Fact, Harmonize, tambua kua asiyeweza kuumba hawezi kuumbua, Mwenyezi Mungu pekee ndio mwenye kazi ya kutoa kasoro na kuumbua sababu ni mungu wa haki, wewe piga kaziiii Konde.

 

Sina haki wala mamlaka ya kumtoa kasoro H-Baba juu Harmonize, sababu najua madhara waliyopata marafiki wa nabii Ayubu, kipindi cha majaribu yake, nawazungumzia marafiki hawa; Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi.

 

Wanadamu tunakuwa wepesi kusahau na kuhukumu kuliko mungu, lakini maandiko yametupa nuru na hekima ya kuacha kazi ya kumshushaa mtu au kusema wanadamu sababu Mungu pekee ndio huinua na kuwashusha wanadamu. na si sababu ya chawa mmoja wa kisukuma.

 

Tanuru hupima kazi ya mfinyazi, ndivyo pia mazungumzo yanavyopima mtu.matunda huonyesha mti ulivyotunzwa vivyo hivyo maneno ya mtu humjulisha alivyo. Soma mstari huu kwa herufi kubwa na kwa tafakuri> [1 Timotheo 3:2].

 

Biblia/Qur-an ina kila kitu na kila kitu kipo kwenye Qur-an/Biblia, ukiweza fasiri maana ya mafundisho yaliyomo kwenye Qur-an/Biblia utajua kweli na kweli itakuweka huru, utamuogopa Mungu pekee na kujiandaa kufa kifo chema na cha busara kwa kusudi lake.”

Leave A Reply