Agnes Almasy wa ITV Kuagwa Leo

ALIYEKUWA mwandishi na mtangazaji wa ITV, Agnes Almasy, anatarajiwa kuagwa leo Septemba 5, 2020, jijini Dar es Salaam na baadaye mwili wake utasafirishwa kupelekwa jijini Tanga kwa ajili ya maziko.

 

Akizungumza kwa niaba ya familia, shangazi wa marehemu, Rose Almasy, amesema kuwa marehemu Agnes ambaye alifariki ghafla juzi akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Amana ataagwa kesho katika kanisa la Anglican Buguruni na baadaye wataanza safari ya kuelekea Tanga.

 

“Maandalizi yanaendelea baina yetu familia pamoja na kampuni aliyokuwa akifanyia kazi; tutampumzisha mpendwa wetu Tanga,” alisema.

 

 

Agnes alihitimu Stashada katika Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam, ambapo baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Lovely Professional University kilichopo nchini India na kupata Shahada ya Uandishi wa Habari na Umma mwaka 2017.

 

Aliajiriwa  katika kituo cha utangazaji cha ITV Machi 19, 2018, akiwa mwandishi wa habari. Marehemu Agnes ameacha mume na mtoto mmoja wa kike.

 

Mungu ailaze roho ya marehemu Agnes Almasy mahali pema. Amina.

Toa comment