The House of Favourite Newspapers

MWILI WA ALIYEKUWA MKE WA MZEE MENGI WAWASILI DAR – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameungana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Media group, Dkt. Reginald Mengi, familia, ndugu, jamaa na marafiki kuupokea mwili wa aliyekuwa mke wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini, marehemu Bi. Mercy Anna Mengi,  ambao umewasili mchana huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.

Mwili wa Bi. Mercy ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa IPP Media, umewasili leo Jumatano, Novemba 7, 2018 ukitokea nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hosptali ya Mediclinic Morningside ya Johannesburg kabla ya kukumbwa na umauti Oktoba 31 mwaka huu.

Mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo iliyopo Mwenge Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Marehemu anatarajiwa kuagwa  kesho baada ya ibada itakayofanyika katika kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam majira ya saa 6:00 mchana kisha kusafirishwa kwenda Machame, Moshi, Kilimanjaro kwa ajili ya maziko ambayo yatafanyika Jumamosi, Novemba 10, 2018.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO

Comments are closed.