Likwalile kuzikwa leo Mpiji-Magoe

MWILI wa katibu mkuu wa zamani wa wizara ya fedha na mipango nchini Tanzania, Dk. Servacius Likwelile, unazikwa leo Jumanne tarehe 23 Februari 2021, Mpiji, Magoe, jijini Dar es Salaam.

 

Likwalile, alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi, tarehe 20 Februari 2021, katika Hospitali ya Regency, jijini Dar es Salaam.

 

Jana mwili wa ofisa huyo aliyewahi kuwa kuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ulilala nyumbani kwake, Mbweni.

 

Asubuhi ya leo utapelekwa Kigango cha Mtakatifu Yohane Mbatizaji Ndege Beach/Mbweni ambapo pia, kutafanyika shughuli ya kumwombea na kumuaga.

 

Baada ya hapo utapalekwa Mpiji Magoe, kwa maziko.

Toa comment