The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Edward Lowassa kuzikwa Feb 17 kijijini kwao Ngarash, Monduli Arusha

0

Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowassa unatarajiwa kuzikwa Februari 17, 2024 kijijini kwao Ngarash wilayani Monduli Mkoa wa Arusha.

Taarifa kuhusu maziko yake,
iliyotolewa leo Februari 11, 2024 na msemaji binafsi wa Lowassa, Aboubakar Liongo nyumbani kwa mwanasiasa huyo, Masaki jijini Dar es Salaam imebainisha kuwa ratiba rasmi ya mazishi itaanza Februari 13, 2024 itakayohusisha taratibu zote za kiserikali.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa waombolezaji wataondoka Dar es salaam kuelekea Arusha siku ya Alhamisi ambapo msiba utahamia Arusha.

Lowassa alifariki Dunia Februari 10, 2024 majira saa 8 mchana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango jana, Lowassa alifikishwa katika taasisi hiyo baada ya kuugua shinikizo la damu, matatizo ya mapafu na
kujikunja kwa utumbo.

“Taarifa zaidi kuhusu mazishi itatolewa baadaye, lakini kwa sasa maziko yatafanyika Ngarash Monduli mkoani Arusha siku ya Jumamosi, Februari 17, 2024 saa 8 nmchana,” amesema Liongo.

Leave A Reply