Mwili wa Hans Pope Waagwa Dar (Pichaz + Video)

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usaji ya Simba Sc na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Zacharia Hanspope umeagwa leo Jumatatu, Septemba 13, 2021 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Zoezi hilo limehudhuriwa na  viongozi mbalimbali wa vilabu vya Simba, Yanga, vilabu vingine vya Soka, viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), viongozi wa Serikali bila kusahau wadau na mashabiki wa masuala ya mpira walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu hans.

Hans Pope alifariki dunia usiku wa Ijumaa, Septemba 10, 2021 katika Hospitali ya Agha Khan alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kesho mwili wa Hans Pope utaagwa nyumbani kwake maeneo ya Ununio jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa maziko.702
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment