The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Kofi Annan Wawasili Ghana, Kuzikwa Alhamisi – Picha

RAIS wa Ghana, Nana Akufo-Addo ameongoza mamia ya waombolezaji kuupokea mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Kofi Atta Annan (80) uliowasili nchini humo ukitokea Jijini Geneva nchini Uswisi jana Jumatatu, Septemba 11, 2018.

 

Annan aliyewahi kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel (2001), alifariki Agosti 18 mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi. Annan aliongoza Umoja wa Mataifa kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2006.

 

Aidha, aliwasili mkoani Mbeya (Tanzania) mwaka 2011 na kuitembelea taasisi ya ARI UYOLE inayojihusisha na masuala ya uboreshaji wa kilimo na utafiti katika nchi za Afrika.

Annan anatarajiwa kuzikwa kitaifa nchini humo keshokutwa Alhamisi huku maelfu ya waombolezaji na viongozi kutoka nchi mbalimbali wakitarajiwa kuhudhuria shughuli hiyo ya kumsindikiza mwanasiasa huyo mkongwe wa Bara la Afrika katika nyumba yake ya milele.

Comments are closed.