MWILI WA MAMA’KE SHIGONGO KUZIKWA LEO!

MWILI wa mama mzazi wa Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, Bi. Asteria Kahabi aliyefariki dunia Julai 27, mwaka huu unatarajiwa kuzikwa leo.

 

Mazishi ya Bi. Asteria yanatarajiwa kufanyika katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosha wilayani Sengerema, Mwanza ikiwa ni baada ya jana kuagwa nyumbani kwake Nyakato Mecco.

Awali, Jumapili iliyopita Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli alifika nyumbani kwa marehemu Mikocheni B jijini Dar na kumfariji Shigongo kisha baadaye mwili wa Bi. Asteria kuagwa na kusafirishwa kuelekea jijini Mwanza.

Viongozi waliopata nafasi ya kufika nyumbani kwa marehemu Mikocheni B kabla mwili haujasafirishwa na kumfariji Shigongo na familia yake ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Mikocheni B, Mbunge Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

 

Watu wengine mashuhuri waliofika msibani hapo ni Asha Baraka, Masanja Mkandamizaji, Faidha Omary ‘Sister Fay’ pamoja na wengine wengi.


Toa comment