The House of Favourite Newspapers

MWILI WA MAREHEMU RUGE UMEWASILI NCHINI

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukitokea Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu. Sasa ni safari ya kuelekea Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa kabla ya taratibu za kuagwa kesho. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alikuwa mmoja wa watu waliofika kuupokea mwili huo.

Mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ukiwa katika gari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
….Ulipokuwa unatoka ndani ya uwanja wa ndege upande wa mizigo.
…Polisi akiongoza msafara uliochukua mwili wa marehemu Ruge Mutahaba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto mwenye kanzu) akifanya mawasiliano.
Watu wakiwa katika uwanja wa ndege kabla ya mwili kufika.

PICHA: DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.