The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Masogange Ukitolewa Hospitali Baada ya Kufariki – Video

Mwili wa Msanii wa filamu za Kibongo na video queen maarufu, Agness Gerald Masogange ukitolewa katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada kufariki ghafla leo.

 

Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinadai Masogange alifikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na homa ya matumbo na tatizo la kupungukiwa na damu.

 

VIDEO: TAZAMA VIDEO HIYO

 

Video ya kwanza ya Masogange ilikuwa ni My Lady ya Suma Rider wa Ilalazone, nyimbo ambayo ili-hit sana, nyimbo ambayo pia ilitengeneza historia ya Adam Juma wa Visual Lab kushika camera kwani ilikuwa ni project iliyokuwa chini ya Eddie Juma ambaye ni mtu wa karibu wa Adam.

 

Ikumbukwe, wakati huo Adam Juma alikuwa na graphics designer na editor, hivyo alitumia nafasi ya nyimbo hiyo ku shoot mwenyewe, kwani mwanzo alikuwa akitumia camera man wengine, hiyo ilikuwa ni kabla ya wimbo wa Masogange wa Belle 9.

 

Suma Rider _ My Lady

 

Comments are closed.