The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mch. Mtikila wawasili Karimjee kuagwa

0

Mch. mtikila

Mchungaji Christopher Mtikila enzi za uhai wake.

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila tayari umewasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na wananchi.

Mtikila alifariki dunia Jumamosi iliyopita saa 11:45 alfajiri baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani.

Leave A Reply