Mwili wa Mwanafunzi Aliyeuawa Wakutwa Kichakani

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Yungwe wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita, Alex Pastory amekutwa ameuwawa kwenye eneo la kichaka huku sababu za kifo hicho zikiwa bado azijajulikana.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masono aliomba ruhusa ya kwenda Nyumbani kwao ukerewe kwa ajili ya matibabu kutokana na hali ya afya yake kutokua nzuri.

 

Amesema,marehemu alipewa ruhusa na kuondoka kwenda nyumbani na alivyo maliza matibabu Februari 28, mwaka huu alirejea shuleni na kuendelea na masomo yake.

 

Aidha, Kamanda Mponjoli amesema tangu Machi mosi mwezi huu mwanafunzi huyo alitoweka shuleni pia hakuonekana katika maeneo ya nyumbani ambapo alikua amepanga.

 

Pia, Kamanda amesema ilipofika Machi 8, mwaka huu mama mmoja ambaye jina lake halikujulikana, wakati akiwa shambani analima aliona fuvu la Binadamu kwenye eneo la shamba lake hali iliyomshitua na kupelekea kuwaita wananchi na walipofika na kuchunguza walibaini kuwa ni mabaki ya nguo za shule kuwepo kwenye eneo hilo.

Toa comment