The House of Favourite Newspapers

MWILI WA RCO ILALA WAZIKWA ARUSHA

MWILI wa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala jijini Dar es Salaam, SSP Anael Mbise (48) umezikwa leo Jumamosi, Mei 11, 2019, nyumbani kwao katika Kijiji cha Kikatiti, Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha.

Viongozi mbalimbali wa Serikali vwamehudhuria maziko hayo wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Ganmbo, wakuu wa wilaya, viongozi na maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi, pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Mbise alifariki dunia Jumanne, Mei 7, mwaka huu baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Prado kutokea Same kuelekea Moshi kugongana na basi dogo la kampuni ya KVC iliyokuwa ikitokea Moshi kuelekea Same, eneo la wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro wakati akiwa safarini kuelekea kijijini kwao Kikatiti kwa mapumziko akitokea Dar.

Mwingine aliyefariki katika ajali hiyo ni Frank Macha (35) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni fundi umeme na kujeruhi mmoja ambaye ni Samson Macha (23) Mkazi wa Dar aliyevunjika mguu wa kushoto na anaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Same.


Aidha, akizungumza wakati wa mazishi hayo, Makonda ameahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa familia ya marehemu Mbise ili kusaidia baadhi ya mahitaji kwa watoto wa marehemu.

Makonda ameongeza pia; “Mimi ni mfano hai wa platform inayotembea kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu. Ninapigwa kila aina ya pigo lakini nashinda kwa sababu Kristo ndio tumaini langu. Jana na juzi nilipata nafasi nzuri zaidi ya kumtafakari Mungu kwa kina sana baada ya wimbi ambalo halielezeki lilipotokea, linapotaka kwenda na kusudi lake.”

Mbise ameacha Mjane na watoto wanne ambao ni Erick, Dorcus, David na Mika.

JWTZ Watoa Onyo Kali Wananchi Wanaovamia Maeneo ya Jeshi

Comments are closed.