The House of Favourite Newspapers

MWILI WA RUGE MUTAHABA WAWASILI BUKOBA (PICHA +VIDEO)

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba ukitolewa nje.

Mamia ya wakazi wa Bukoba na vitongoji vinavyoizunguka Wilaya hiyo wamejitokeza kwa wingi kuupokea  Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.
Kamati ya Maandalizi chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inasema imejipanga kuupokea ugeni huo mkubwa.

Waombolezaji wa Mkoa wa Kagera waliojitokeza kuupokea mwili wa marehemu Ruge Mutahaba wakipokea mau kabla ya kupokea jeneza lenye mwili.
Mamia ya waombolezaji waliojitokeza uwanja wa ndege wa Bukoba kuupokea mwili wa Ruge.
Jeneza lenye mwili wa Ruge Mutahaba likipelekwa kwenye gari maalum baada ya kushushwa kwenye ndege tayari kuelekea nyumbani kwao kijiji cha Kiziru
Jeneza lenye mwili wa Ruge Mutahaba baada ya kufika nyumbani kwao Bukoba Kijiji cha Kiziru.
Waombolezaji wakiweka vizuri maua yaliyoandaliwa.
Wakazi wa Bukoba walivyoupokea mwili wa Ruge Mutahaba.
Taswira ilivyoonekana maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Waombolezaji wakiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Kagera wakisubiria mwili wa marehemu Ruge uwanja wa Ndege wa Bukoba.

 

(Picha na Abdullaif Yunus  Global Publishers, Bukoba)

Comments are closed.