The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Semwanga Wawasili Uganda kwa Mazishi

0
Ivan Semwanga (kushoto) alipokuwa amelazwa hospitalini Afrika Kusini na kulia wakati wa uhai wake.

IVAN SEMWANGA, aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘The Bosslady’ ambaye sasa ni mpenzi na mzazi mwenzake wa mwanamuziki wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnum’, atazikwa Jumanne (Mei 30) wiki ijayo  nyumbani kwao Kayunga, Uganda.

Semwanga akiwa na Zari wakati wa ndoa yao.

Mwili wa mwananchi huyo wa Uganda aliyefariki nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya moyo, umewasili leo nchini Uganda ambako leo utafanyiwa mkesha maalum na Jumatatu kufanyiwa ibada maalum ya wafu katika Kanisa la Namirembe siku ya Jumatatu.

Semwanga alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

 

Leave A Reply