The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Waziri Kissinger wa Njenje Watolewa Mochwari

0

MWILI wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini Waziri Ally Kissinger umetolewa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya maziko.

Marehemu Waziri alifariki dunia jana Ijumaa, Julai 23, 2021 katika Hospitali hiyo usiku huku familia ikitaja chanzo cha kifo chake kuwa ni malaria na alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

Enzi za uhai wake marehemu Waziri alifanya kazi katika bendi mbalimbali ikiwemo Msondo Ngoma na nyingine nyingi na kupata umaarufu zaidi akiwa na bendi yake ya Kilimanjaro maarufu kwa jina la Wana Njenje, ambayo ndio alikuwa anaitumikia mpaka umauti ulipomkuta.

Mwili wa marehemu Waziri Njenje unatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwao Pongwe Mkoani Tanga.

Live: Misa Ya Kumbukumbu Ya Mwaka Mmoja Wa Kifo Cha Hayati Mkapa

Leave A Reply