The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Waziri wa Kwanza wa Elimu ‘Thabitha Ijumba’ Ulivyoingizwa Kanisa KKKT Msasani

Dar es Salaam, 15 Machi 2025: Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Kwanza katika Kipindi cha Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, muda huu umeingizwa katika Kanisa la KKKT Msasani jijini Dar, alipokuwa akisali kipindi cha uhai wake.

Baada ya ibada ya mazishi mwili huo unatarajiwa kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Miongoni mwa waliohudhuria kwenye ibada hii ni viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wastaafu na wengineo. Ibada imeshaanza kwa nyimbo za maombolezo.

Marehemu Thabita enzi za uhai wake.

HABARI/PICHA; NA RICHARD BUKOS /GPL