Mwimbaji Ekwueme Azikwa Baada ya Miezi 2, Mumewe Asusia Mazishi

Hatimaye Osinachi amezikwa baada ya miezi miwili

OSINACHI Nwachukwu; ni aliyekuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria ambaye hatimaye jana amezikwa baada ya miezi miwili tangu kifo chake.

 

Mwili wa Osinachi umelazwa kwenye nyumba yake ya milele katika mji aliozaliwa wa Isochi Umunneochi katika Jimbo la Abia nchini Nigeria.

 

Osinachi alifariki dunia Aprili 8, 2022 huko Abuja akidaiwa kuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani kabla ya kifo chake.

Osinachi enzi za uhai wake

Kifo chake kilihusishwa na mumewe, Peter Nwachukwu ambaye ameshtakiwa kwenye Mahakama Kuu ya Jimbo Kuu la Shirikisho.

 

Mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu, hakuwepo katika mazishi yake huku mtoto wa kwanza wa Osinachi akidai kuwa baba yake aliwafahamisha kuwa kuwapiga na kuwatesa wanawake ni njia inayokubalika maishani.

 

Cc; @sifaelpaul3471
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment