#GlobalCelebrityUpdates: Hii Ndio Hobby Kubwa Ya Msanii Akothee Kutoka Kenya… Sio Kuimba

Esther Akoth maarfu kama Akothee anafahamika kama mwanamziki wa kike mwenye hela zaidi Kenya. Ujio wake kwenye muziki umekuja na stori nyingi sana juu ya maisha yake, na leo nimekutana na hii inayotrend mitandaoni kwa Kenya.

Akothee ni mwanadada mwenye sotri nyingi, iwe muziki au biashara zake msanii huyo kutoka Kenya ni miongoni mwa mastaa wanoongoza kwa kuleta gumzo na tetesi nyingi sana kwenye tasnia ya muziki Nairobi.

Kwenye kupitapita kwangu kwenye Instagram asubuhi hii nimekutana na post moja ya Akothee inayotrend vilivyo kwenye blogs na websites kadhaa Kenya. Akothee ameweka wazi kuwa very soon atamkaribisha kwenye familia yake mtoto wake wa sita. Hii ni zaidi ya miezi 6 baada ya kupoteza mimba yake ya mwisho!

Kupita page yake ya Instagram @Akotheekenya, msanii huyo alipost picha ya waoto wake wawili na kuweka caption inayosema:

Hobby yangu kubwa ni kuzaa, kubali kataa, hakuna cha kunishinda baby no.6 yupo njiani,baby daddy mtamjua tuu hayo ni maamuzi yangu ya maisha, chagua vita yako” – Akothee.

Picha yenyewe hii hapa chini…

Una chochote cha kushare kuhusu hiki? Niachie comment yako hapa chini.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.
Toa comment