Mwingine Akutwa na Corona Dar, Wagonjwa Wafikia 20
WIZARA ya Afya leo Jumatano, Aprili 1, 2020 imethibitisha kuwepo kwa kesi ya mpya maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19) nchini iliyopatikana jijini Dar es Salaam. Mgonjwa huyo ni raia wa Marekani, mwanamke mwenye miaka 42. Hadi sasa kesi zilizodhibitishwa hapa nchini ni 20.
“Wizara ya Afya inathibitisha kuwepo kwa Kesi Mpya ya ya maambukizi ya Virusi vya Corona Nchini iliyopatikana Jijini Dar es Salaam. Mgonjwa huyo ni raia wa Marekani,mwanamke Mwenye miaka 42.Hadi sasa Kesi zilizodhibitishwa hapa nchini ni 20,” amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.