WAZIRI wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu, amesema kuwa mgonjwa mwingine aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini amepona.
Amesema hayo leo Ijumaa, Aprili 03, 2020 katika taarifa aliyoitoa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwemo akaunti ya Twitter na Instagram kwamba mgonjwa aliyekuwa Ngara mkoani Kagera amepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa watatu.
“Mungu ni mwema. Na leo pia hatuna case mpya za COVID19. Mgonjwa wa Kagera (Ngara) amepona. Sasa jumla ya waliopona ni 3,” ameandika waziri huyo.
“Mgonjwa aliyebaki wa Arusha vipimo vyake siku ya 9 leo ni Negative. Tutampima siku ya 14 ili kujiridhisha kama amepona. Wagonjwa wengine 15 waliobaki wanaendelea vizuri,” amezidi kueleza.
Ametoa rai kwa wananchi kuepuka misongamano na mikusanyiko na kufuata maelekezo ya wataalam ili kujikinga na maambukizi hayo.
Mungu ni mwema. Na leo pia hatuna case mpya za COVID19. Mgonjwa wa Kagera (Ngara) amepona. Sasa jumla ya waliopona ni 3. Mgonjwa aliebaki wa Arusha vipimo vyake siku ya 9 leo ni Negative. Tutampima siku ya 14 ili kujiridhisha kama amepona. Wengine 15 waliobaki wanaendelea vzr pic.twitter.com/DcZVFTKrt1
— Ummy Mwalimu, MP (@umwalimu) April 3, 2020