The House of Favourite Newspapers

Mwinyi Achukua Fomu ZEC, Aahidi Zanzibar Mpya – Video

0

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein  Mwinyi amechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti hicho ambapo  amekabidhiwa  na Jaji Mkuu (Mst.) Hamid Mahmoud Hamid ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

 

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo, katika ofisi za ZEC, Mwinyi amesema atahakikisha anaondoa matabaka ya kila aina, matabaka ya Upemba na Uunguja, Ukusini na Ukaskazini na matabaka ya dini zote ili kujenga Zanzibar mpya na kila mmoja kunufaika na maendeleo ya Zanzibar.

 

Aidha, ametoa wito kwa Wazanzibari wote kuhakikisha wanalinda amani na utulivu ili kufikia malengo ya kujenga Zanzibar mpya itakayowanufahisha Wazanzibari wote bila kubagua mtu.

 

“Iwapo mtanichagua kuwa kiongozi wenu nitahakikisha tunajenga uchumi wa kisasa, na hivyo kufikia uchumi huo vijana muwe tayari kuajiriwa popote ili kuinua uchumi wetu,” amesema.

Amesisitiza kujenga miundombinu rafiki itakayoleta mazingira mazuri kwa wananchi  ili kufikia uchumi wa kisasa na kunufaika na uchumi huo.

 

Katika hatua nyingine amesema  atahakikisha mapato yanakusanywa kwa ufasaha bila kupotea ili mapato hayo yakatekeleze miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

 

“Hivyo basi viongozi wa chama na wanachama wote sasa ni wakati wa kuingia kazini ili kuhakikisha chama kinapata ushindi katika uchaguzi huu kwani uchukuaji fomu ndiyo kiashiria cha kipenga cha uchaguzi kupulizwa rasmi,” amesisitiza.

 

Mwinyi ametamatisha kwa kuwataka Wazanzibar wote kujitokeza siku ya kupiga kura Oktoba 28, mwka huu ili kuhakikisha chama kinapata ushindi kwa kishindo kikubwa. 

KAULI ya DKT HUSSEIN MWINYI BAADA ya KUCHUKUA FOMU – “NAKUJA NA STAILI YA MAGUFULI”

Leave A Reply