MWISHO WA UBISHI… MAN FONGO ALIVYOKINUKISHA DAR LIVE

WAPENZI wa burudani usiku wa kuamkia leo walipata uhondo wa aina yake ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live wakati wakali wa kutoa burudani, Man Fongo na Sholo Mwamba pamoja wakali wengine walipoonyesha makali yao.

Katika tamasha hilo lililotambuliwa kwa jina la Mwisho wa Ubishi, hudhuriwa umati wa mashabiki ilikuwa ni mwendo wa ‘kukata kilaji’ na kuserebuka mwanzomwisho.

Burudani ya muziki ukumbini hapo ilifunguliwa na Yah Taarab, ambao waliachia vibao vyao vipya na vinavyoendelea kutamba na kuwanogesha mashabiki.

Baada ya hapo wakaingia Jahazi Modern taarab waimbaji wake ambao walidatisha lakini zikiwa na ustaarabu wa kimaadili na kunogesha mambo ukumbini.

 

Wapenzi wa burudani wakati wakiendelea kupiga mayowe ya kumshangilia ‘Chura’ mkali wa Singeli kutoka pande za Uswazi, Man Fongo aliingia na kubadilisha mandhari kwa staili yake ya singeli.

 

Baada ya Man Fongo kuwapeleka puta mashabiki, Mwisho wa siku akapanda Sholo Mwamba ambaye pia alifanya yake.

PICHA/ STORI: SUNDAY BUSHIR / GPL


Loading...

Toa comment