MWISHO WA UBISHI… SHOLO MWAMBA AANDIKA HISITORIA

MKALI wa Muziki wa Singeli Bongo, Sholo Mwamba usiku wa kuamkia leo ameandika historia ya aina baada ya kupiga bonge la shoo lilokwenda kwa jina la MWISHO WA UBISHI ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Katika shoo hiyo iliyoandaliwa na Dar Live wenyewe, kulishuhudiwa wakali wa kutosha wakipanda jukwaa moja la Dar live na kuamsha popo mwanzo mwisho.

Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na maelfu wa mashabiki wa muziki huo, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea maadhimisho ya kumbukumbu ya Sikukuu ya Kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka).

Shoo hiyo ilianza mida ya saa mbili kwa wakali hao kupanda huku burudani ya kipekee kwa madensa ikigeuka kivutio kikubwa kwa mashabiki waliohudhuria.

Miongoni mwa waliokinukisha katika shoo hiyo, YAH Tmk Taarab, Jahazi Modern Taarab, man Fongo na wengine wengie.


Loading...

Toa comment