The House of Favourite Newspapers

Mzava asema Mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na mwekezaji ni wa miaka na miaka, Silaa aombwa Kuingilia kati

WANANCHI wa Vijiji vitano vya Lewa, Mgobe, Kalekwa, Lewa na Werei vilivyopo Kata ya Magila Gereza wilayani Korogwe wameelezea marumaini yao juu ya ujio wa Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi Jerry Slaa kuwapatia suluhisho juu ya mgogoro unaofikuta kati yao na Mwekezaji wa Shamba la Sufi Limited

Hatua hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Tanga, Rajabu Abdarahman Abdallah kufika kwenye Kijiji cha Mgobe ambapo baada ya kuzungumza na wananchi wa vijiji yenye mgogoro alitoa maagizo.

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Timotheo Mzava alisema, mgogoro huo umefukuta kwa muda mrefu na ulijitoleza baada ya mwekezaji huyo wa shamba la Sufi Limited kutoliendeleza eneo lake kwa muda mrefu hali ambayo ilisababisha wananchi wenye changamoto ya ardhi kuvamia ili kuendesha shughuli zao za Kilimo.

Mzava alisema kwamba wanamshukuru Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati kuu kutoa maagizo kwa Waziri wa ardhi ili aweze kuja kwenye kata hiyo ya Magila Gereza kushughulikia mgogoro huo wa ardhi.

Inaelezwa kuwa mgogoro huo ulianza tu mara mwekezaji alipohitaji kutumia tena eneo lake hilo katika kipindi ambacho tayari wananchi walikuwa wamejitwalia maeneo wakiendesha shughuli zao.

“Haya maeneo ni mashamba ya mwekezaji na mwekezaji kwa muda mrefu alipotea na wananchi wakaingia kuendesha shughuli zao baada ya kukosa maeneo” alisema Mzava huku akielezea matumaini yake juu ya kupatikana suluhu juu ya changamoto hiyo.

Mzava alisema kwamba, iwapo maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga yatatekelezwa kwa Waziri wa ardhi kufika eneo hilo Wananchi wa Mgobe na mwekezaji kila mmoja ataweza kuendesha shughuli zake kwa amani.

Mzava alieleza kwa walijitahidi kufanya jitihada mbalimbali kutatua mgogoro huo ambapo waligonga mwamba na hivyo sasa wanasubiri ujio wa Waziri wa ardhi wakiamini kuwa atajua kiini cha tatizo na kupata suluhu ili amani kutawala.