The House of Favourite Newspapers

Mzee Akilimali Aingilia Ishu Ya Chirwa

Ibrahim Akilimali.

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amemtetea mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kufuatia kukosa penalti katika mechi ya juzi dhidi ya URA ya Uganda kwenye Kombe la Mapin­duzi.

 

Yanga iliondolewa katika nusu fainali kwa penalti 5-4 ambapo Chirwa alikosa kwa upande wa Yanga na kusaba­bisha kuwa gumzo kutokana na tukio hilo.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Akilimali alisema Chirwa hakufan­ya makosa katika kupiga penalti ya mwisho kwani alidhamiria kufunga na kilichotokea ni bahati mbaya na kudai kuwa, kocha ndiye anayepaswa kulaumiwa kutokana na kumtumia licha ya kutokuwa na ma­zoezi ya pamoja na wenzake.

 

“Yanga tumetolewa kiume katika michuano ya Mapinduzi kwani hadi tunatoka tumefanikiwa kufanya vyema hadi dakika 90 lakini kili­chotokea hakipaswi kulaumiwa mchezaji.

 

“Timu ilicheza vizuri ilipamba­na na hatimaye kuweza kufikia hapo tulipofikia na ilikuwa ni lazima timu moja isonge mbele.

 

“Siwezi kumlaumu Chirwa, kilichotokea ni bahati mbaya kwani, hata wachezaji wa­zuri Ulaya wanakosa penalti sembuse yeye, anayepaswa kulaumiwa ni kocha kwanini amemchezesha mchezaji akiwa hana mazoezi, naona anayarudia yaleyale ya Kocha Hans Pluijm,” alisema Akilimali.

Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam | Championi Ijumaa

Comments are closed.