The House of Favourite Newspapers

Mzee Akilimali, Hili La Yanga Linakuhusu Usijikaushe!

Mwenyekiti wa klabu, Yusuf Manji.

 

TUMEWAHI kusikia kwamba hata wale wanaojiita wazee wa klabu huwa wana ma­slahi yao, pale yanapoguswa tu, basi kunakuwa na tatizo kubwa sana.

 

Mara nyingi, wazee wame­kuwa wakijificha katika mwamvuli wa “tumetoka mba­li na klabu” au ule mwamvuli wa “tuna uchungu na klabu”.

Lakini kunaweza kukawa na ukweli zaidi ya huo kwa kuwa wale wanaopiga kelele sana nao wanakuwa wanafaidika sana pale kunapokuwa na mambo yanayowahusu wa­zee.

 

Mfano wazee wanasikilizwa kwa sababu ya kuheshimi­wa, na wakati mwingine wa­naweza kuzungumza jambo likaonekana halina maana la­kini kivuli cha uzee kikaen­delea kuwalinda.

 


Wapo wazee wa klabu, wanao­nyesha ni wa­zee hasa na wamekuwa hawaingilii mambo ya klabu kama Yanga na Simba na wakati mwingine wametoa ushauri wao chinichini bila ya kuju­likana na ukawa ushauri ambao ni msaada mkub­wa.

 

Wakati fulani kulikuwa na maneno, kwamba mzee Ibrahim Akilimali, aliamua kupishana na uongozi wa Yanga kwa kuwa mwenyekiti wa klabu, Yusuf Manji alionyesha msi­mamo wa juu kabisa.

 

Msimamo wa Manji ili­kuwa ni kusisitiza, baraza la wazee halitambuliki kikatiba, hivyo kutaka wazee hao kubaki kama washauri lakini si chom­bo chenye nguvu ya ku­gombana au kupingana na uongozi.

Lakini kukawa na taar­ifa kwamba wazee huwa kwenye kamati ya ufundi, kamati ambayo huchota fed­ha kila mechi na baada ya kukatwa kwa fedha hizo, ndiyo tafrani likaanza kati ya wazee na uongozi. Hata hivyo, mzee Akilimali ambaye ni katibu wa baraza hilo la wazee, aliwahi kufafanua na kusema habari hizo hazikuwa na ukweli.


Yote yanawezeka­na, ukweli au uongo. Lakini wote mnakum­buka mzee Akilimali alivyokuwa akieleza kwamba Yanga ina fedha za kutosha kui­saidia k l a b u hiyo h a t a baada ya kuondoka kwa Manji.

 

Mzee Ak­ilimali mara kwa mara alisisitiza suala la kuondoka kwa Manji, akisema kuna wawekezaji waliokuwa wanahitaji kuingia Yanga na kuwekeza. Tena akase­ma kulikuwa na fedha ny­ingi, takriban milioni 600 kwa ajili ya maendeleo ya Yanga, ingawa hakusema zi­natokea wapi.

 

Yanga sasa iko katika wakati mgumu, inakosa uon­gozi wa mtu kama Manji ali­yekuwa imara kwa maana ya uongozi, alikuwa na mipango thabiti kwa kuwa ni mfan­yabiashara mkubwa na alijua nini cha kufanya.

L a k i n i Manji ali­weza kui­saidia Yanga kwa kutoa kwa upendo au kukopa kwa kuwa ana uwezo. Yanga hai­kuwa na shida zi­nazotokea leo na mai­sha yalikuwa mazuri.

 

Yanga ilikuwa ni ya ki­mataifa, inayoweka kambi Uturuki na kadhalika. Iliyopan­da ndege kila siku, sasa tangu kuondoka kwa Manji ambaye alionekana hafai na akina mzee Akilimali wakaonyesha hafai, Yanga imevuliwa ub­ingwa wa Kombe la Shirikisho, imevuliwa ubingwa wa Tanza­nia Bara.

 

Bahati nzuri imepata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirik­isho hatua ya makundi, lakini wachezaji wamekuwa wakigo­ma, inasafiri kwa kuunga na hakika maisha ni magumu sote tunaona.

Swali linaanzia hapo, ukimya wa mzee Akilimali kuhusiana na mipango uko wapi? Kipindi kile alikuwa ak­isema na kueleza mambo lukuki, sasa yako wapi?

 

Yanga inateseka, nazikum­bushia zile Sh milioni 600, sasa ndiyo wakati mzuri na zina­hitajika. Wawekezaji aliosema wapo, huu ndiyo muda sahihi mzee Akilimali awalete.


Nimekuwa nikisisitiza, kwamba hizi klabu zinaumi­zwa na wale wenye mata­manio na matakwa binafsi. Wale wanaojiona wamiliki lakini msaada wao ni maneno pekee.

 

Wakati mgumu kwa Yanga, hautadumu milele, iko siku ata­tokea mkombozi na si lazima awe Manji kwa kuwa Yanga haiwezi kuishi na Manji milele. Lakini vizuri wahusika na wenye nafasi za kuzungumza au kuse­ma jambo kuhusiana na klabu muangalie maslahi zaidi yanay­oihusu klabu na si yenu binafsi.

 

Kwenye shida mnakimbia, kukiwa na neema kila siku ma­neno na mnaungana kutaka kuwaonyesha watu wabaya mkisema wanafaidika na klabu na mkitaka kuionyesha jamii, klabu inanyonywa.

 

Sasa klabu hainyonywi? An­galia maisha haya ya shida, kipi bora? Mtu ajifaidishe na klabu ifaidike au kuwe hakuna anaye­jifaidisha na klabu inateseka, inaaibika na kuumiza mioyo ya mamilioni wanaoipenda.

Mzee Akilimali tunakukum­buka, hatujakusahau na tunazi­kumbuka na kuzikumbusha Sh milioni 600 zako. Sema mipa­ngo ya ukombozi ni ipi, usikae kimya Yanga inateseka!

WAKATI fulani kulikuwa na maneno, kwamba mzee Ibrahim Akilimali, aliamua kupishana na uongozi wa Yanga kwa kuwa mwenyekiti wa klabu, Yusuf Manji alionyesha msimamo wa juu

STORI: SALE HALLY

Comments are closed.