Mzee Bayo Amwaga Machozi Mtoto Hatembei, Degedege Inamtesa – “Rais Samia Na Watanzania Nisaidieni”- Video
Ukiona mtu mzima analia mbele za watu, ujue kuna jambo! Charles Bayo analia. Kinachomliza ni mwanaye Emmanuel Bayo (15) ambaye anateseka.
Emmanuel alizaliwa akiwa timamu kama watoto wengine lakini siku nne tu baadaye, mambo yalianza kubadilika na kuanzia hapo, maisha hayajawahi kuwa sawa tena.
Mtoto Emmanuel anatatizo la mtindio wa ubongo, viungo vyake vinakakamaa, anapatwa na degedege mara kwa mara, hawezi kufanya chochote bila msaada.
Hawezi kusimama, hawezi kukaa wala hawezi kula na ameishi hivyo kwa maisha yake yote tangu akiwa na siku nne tu.
Mzee Bayo anawaomba Watanzania wote wamsaidie kwa hali na mali ili mwanaye aendelee kuhudhuria kliniki na kupata matibabu.
Anaomba matatizo alionayo yakamguse Rais @samia_suluhu_hassan ili amsaidie, anaomba watu wote wenye uwezo wamsaidie kwani matatizo aliyonayo ni mazito.
Kama umeguswa na unataka kumsaidia, wasiliana naye kwa simu namba 0789668182 (Charles Bayo).
Tegeta Wazo, degedege, utindio wa ubongo, viungo kukakamaa, 15, Emmanuel Bayo siku nne baada ya kuzaliwa