MZEE JENGUA VIFAA VYA MAITI, VILIOKOA UHAI WANGU !

MKONGWE wa Bongo Movies, Mohammed Fungafunga ‘Mzee Jengua’ amefunguka mengi kuhusu maisha yake binafsi na sanaa kwa jumla ikiwemo tukio la kurogwa na kuokolewa na vifaa vya maiti.
Amani lilimtembelea mkongwe huyo nyumbani kwake, Kigogo- Luhanga jijini Dar, mambo yalikuwa hivi;
Amani: Habari mzee.
Mzee Jengua: Nzuri, karibu nyumbani, una bahati mbaya kwa sababu mke wangu hayupo kasafiri, kaenda Bagamoyo.
Amani: Hakuna neno, hivi ilikuwaje ukajiingiza kwenye uigizaji?
Mzee Jengua: Nilikuwa naipenda sanaa muda mrefu sana, lakini baadaye nilikutana na Mponda, ni mtu wa Kenya ndiye aliyegundua kipaji changu, alinifuata, akaniambia tuanzishe kikundi cha uigizaji, nilimkubalia haraka kwa sababu ni kazi ambayo nilikuwa nikiipenda sana, nakumbuka tulianza watu watano na baadaye tulifanya mchakato wa kwenda ITV na kwa mara ya kwanza, Severine Kiwango na mwenzake walitutembelea wakatushuti demo, ikaenda ITV, mwisho ilikubalika na tukaanza kurusha mchezo mwaka 2000 ambao ulikuwa na dakika tano na uliitwa Chemchem Arts Group, lakini watu walipendekeza mchezo utumie dakika 15, lakini Severine akashauri pia mchezo uitwe Kidedea, tulirusha ITV ndani ya miaka mitatu.
Amani: Mchezo wako wa kwanza kuigiza unaitwaje?
Mzee Jengua: Ulikuwa unaitwa Jirekebishe.
Amani: Mpaka sasa umeshacheza muvi ngapi?
Mzee Jengua: Kiukweli sitaki kujisifu, lakini katika wasanii ambao wamecheza muvi nyingi ni mimi, pia katika wasanii ambao wamecheza tamthiliya nyingi pia ni mimi, ni nyingi siwezi kuzihesabu.
Amani: Sababu gani imewafanya mmeacha kutoa filamu na badala yake mnarekodi tamthiliya?
Mzee Jengua: Soko limeyumba, hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotufanya tuanze kushuti zaidi tamthiliya, zina malipo mazuri kidogo.
Amani: Sanaa ya Tanzania imekunufaisha kiasi gani?
Mzee Jengua: Nimejuana na watu wengi, nimezijua sehemu nyingi sana mpaka nje ya nchi hii na kila sehemu ninayokwenda napokelewa vizuri, kwa hiyo hicho ndo’ kitu kikubwa nilichonufaika nacho katika sanaa.
Amani: Changamoto zipi unazozipata ukiwa lokesheni?
Mzee Jengua: Ni mavazi ya ajabu kwa hawa dada zetu, yaani unakuta binti amevaa kinguo kifupi hakieleweki, sasa mimi nimetokea kupinga pale ambapo naona wasichana wanavaa nguo ambazo hazina maadili ya taifa letu.
Amani: Ni kitu gani kibaya ambacho kimewahi kukutokea lokesheni ambacho hutakisahau?
Mzee Jengua: Nakumbuka nilikuwa sehemu moja Mang’ola (Morogoro) nashuti filamu mimi kama mchawi, nimemuibua mtu kwenye bwawa halafu nikaruka naye juu na kupotea naye. Baada ya kufunguka kipengele kingine ikaonekana kwamba nipo naye nyumbani ni ndondocha, sasa ‘maedita’ wakawa ‘wameediti’ hicho kipande walikuwa na kawaida ya kuweka TV nje usiku halafu wanaonesha vile vipande tulivyoshuti, basi nimelala asubuhi kuamka nikapigwa kitu (kurogwa), nikazimia siku nne, baadaye mke wangu alipokuja nilipelekwa hospitalini nikachomwa sindano 16 na dripu sita, lakini sikuzinduka, mpaka mzee Msisiri (naye mwigizaji) akanitanifutia shekhe akanifanyia dua, ndiyo nikazinduka.
Lakini shekhe alituambia matibabu kamili tuende tukayafanyie Dar, nilipofika Dar ikaonekana matibabu yangu baada ya kusomewa kisomo ilitakiwa vinunuliwe vifaa vya kuoshea maiti kabisa, mkeka sanda na kila kitu ndiyo nikatolewa huyo mdudu.
Amani: Tofauti ya sanaa ya zamani na sasa ni ipi?
Mzee Jengua: Unajua zamani sisi unapochaguliwa ucheze sehemu moja, tulikuwa tunafanya ‘riheso’ wasanii kama watatu.
Amani: Mbali na sanaa unafanya shughuli gani nyingine?
Mzee Jengua: Nina kipaji cha kuchezea nyoka, kwa hiyo huwa nafanya maonesho sehemu mbalimbali, pia ni mfugaji mzuri wa kuku na biashara zangu zingine.
Amani: Ahsante sana mzee kwa muda wako.
Mzee Jengua: Karibu sana.
wanne katika nafasi moja, tofauti na siku hizi mtu akikuona mzuri au ametokea tu kukupenda anakwambia cheza mhusika mkuu.
Amani: Tumezoea kuwaona wasanii vijana tu mitandaoni, ninyi wazee mpo wachache sana, kwa nini?
Mzee Jengua: Ni life style (mtindo wa maisha) ambayo tumejichagulia, nilifunga akaunti yangu muda mrefu baada ya kuona kuna mambo ya kijinga, watu wanatukanana, wanavaa nusu utupu.
Amani: Kuna changamoto gani mtaani kwako?
Mzee Jengua: Watu wengi wanafikiri ninavyoigiza ndivyo nilivyo wakati siyo, kuna watu mpaka leo nikikutana nao wananikimbia kwa kuhisi mimi ni mchawi kweli.
Amani: Msanii gani wa Bongo Fleva ambaye unamkubali?
Mzee Jengua: Nampenda sana Diamond kuliko msanii yeyote Tanzania, anajua kuimba, anajua kulitumia jukwaa vizuri tofauti na yule mbana pua, yaani simuelewagi kabisa (anacheka).
Amani: Mbali na sanaa unafanya shughuli gani nyingine?
Mzee Jengua: Nina kipaji cha kuchezea nyoka, kwa hiyo huwa nafanya maonesho sehemu mbalimbali, pia ni mfugaji mzuri wa kuku na biashara zangu zingine.
Amani: Ahsante sana mzee kwa muda wako.
Mzee Jengua: Karibu sana
Makala: Memorise Richard


Comments are closed.