The House of Favourite Newspapers

Mzee Kambi ‘Amlipua’ Manara, Watoto wa ‘Kamwene’ Hawakustahili – Video

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Mzee Hashim Kambi, amedai kua kitendo cha waandaaji wa Tuzo za Sinema Zetu International Festivals (SZIFF) kuwapa tuzo ya Waigizaji Bora, watoto Flora na Rashid, hakikuwa cha kiungwana kwani katika hali ya kawaida tu ni ngumu watoto hao kuwashinda waigizaji wakubwa kama vile Gabo, Wema, Johari.

 

Mzee Kambi amesema watoto hao walipaswa kupewa tuzo ya wasanii bora chipukizi na si kuwapa tuzo ya waigizaji bora kutokana na umri wao, lakini hata kama ni kuhesabu kura walizopigiwa na mashabiki basi hawana umaarufu wala uwezo wa kuwashinda wakina Wema na Gabo.

 

Aidha, Mzee Kambi ameongeza kuwa hapendezwi na kitendo kinachofanywa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, cha kuisifia Simba mara zote anazoitwa katika tuzo hizo kwa ajili ya kumkabidhi mshindi tuzo yake.

VIDEO: MSIKI MZEE KAMBI HAPA

Comments are closed.