MZEE MAGALI Awashangaa Bongo Muvi

MSANII wa Bongo Muvi aliyehamishia makazi yake Chicago nchini Marekani, Charles Magali ameshangazwa na mastaa wakubwa wa filamu kugalagazwa na watoto kutoka mkoani Iringa, Frola Kihombo na Rashid Msigalla katika Tuzo za Filamu za Kimataifa za SZIFF.

 

Mzee Magali amesema wasanii wa Bongo Muvi waache kubweteka na ustaa wao na kusahau kujituma maana wasanii wanaochipukia wanakuja kwa kasi na wakizidi kubweteka wataendelea kulialia kuonewa kila kukicha.

 

“Nimesikia tuzo kubwa kama ya Msanii Bora wa Kiume na Msanii Bora wa Kike imekwenda kwa watoto hao ambao walikuwa hawajulikani, kwa kweli mastaa wanatakiwa kujiongeza na si kuishia kuwalaumu waandaaji,” alisema.

 

Mkali huyo anayetisha kwa uigizaji wa kibabe, hivi karibuni anatarajia kurudi nchini na kuweka mikakati ya kuiinua tasnia hiyo.

Toa comment