The House of Favourite Newspapers

Video: Mzee wa Miaka 76 Amekuja na Sharti Jipya la Mke Anayemtaka, Wanawake Waanza kuchuana kwa Kasi

athumani
 DAR ES SALAAM: MZEE Athuman Mchambua (76), mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar es Salaam ambaye amezua gumzo mtaani  baada ya kuamua kutafuta mwanamke wa kuoa kwa kuweka bango nyumbani kwake la kutafuta mke na kuandika sifa za mke anayemtaka, ameongeza sharti jipya kwa mke anayemuhitaji.
Amesema licha ya kupokea simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali nchini, lakini amewataka wanawake ambao atawafanyia usaili, hasa kwa yule ambaye atakuwa ameshinda, kutobweteka kwani atakuwa katika kipindi cha mpito cha ndoa yake.
Ikiwa zimebaki siku mbili za kutuma maombi ya kuolewa naye (yaani mwisho wa kutuma maombi ni Jumamosi Desemba 10), mzee huyo ameeleza kuwa mwanamke atakayebahatika kufuzu usaili huo na kukidhi vigezo, atakaa naye kwa muda atampa probation period (muda wa matazamio) wa miaka mitatu.
Mzee huyo ameeleza kuwa amefikia hatua hiyo ili kuanza kupitia majina ya wanawake zaidi ya 30 ambao tayari mpaka sasa wameshatuma maombi wakijaribu bahati ya kuolewa naye.
Alisema kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuweka tangazo hilo kwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaojitokeza hushindwa kukidhi vigezo anavyovihitaji.
Alivitaja vigezo sita muhimu vya mwanamke anayemuhitaji kuwa ni awe mcha Mungu na mwenye uwezo wa kutunza watoto wake.
“Vigezo vingine awe na sifa ya ndoa, awe na sifa ya mume, awe na sifa ya kilimo, awe na sifa ya kutunza watoto na awe na sifa ya usafi wa hali ya juu.
“Tangu kuanza nimepata wanawake zaidi ya 30 ambao wanne kati yao wamefika hapa nyumbani kwangu, lakini wengine wamekuwa wakiona aibu kuja hapa moja kwa moja na hivyo wamekuwa wakitumia simu. Leo (jana) nimewafanyia usaili wanawake watano kwa simu, lakini hakuna hata aliyefuzu nusu ya vigezo, wengi wamekuwa wakiteleza sifa ya kilimo,” alisema.
halotel-strip-1-1

MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

Comments are closed.