The House of Favourite Newspapers

Mzee Yusuf: Eti Nimerudi Mjini Sishtui?

0

MFALME mwenye Taarab yake Bongo, Mzee Yusuf anasema kuwa, watu wanaomsema kuwa amerudi mjinilakini hashtui, ni wale ambao mashabiki wake wa kweli.

 

Akipiga stori mbili-tatu na IJUMAA SHOWBIZ, staa huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Nimerudi Town anasema kuwa, asilimia kubwa ya watu wanaoongea kuhusu kufeli kwake baada ya kutangaza kurudi mjini, siyo mashabiki wake kindakindaki na wala huwa hawafuatilii shoo zake kwa sababu kama wangekuwa wanafanya hivyo wasingekuwa wanaongeaongea.

 

“Wanasema nimerudi mjini sishtui? Unajua hao watu wanaokesha kunisema kuwa kwa sasa sishtui, mimi wala siwashangai kwa sababu naamini kabisa siyo mashabiki wangu na wala kwenye shoo zangu huwa hawahudhurii kabisa ndio maana wanakuwa na maneno mengi, laiti kama wangekuwa wananifuatilia vizuri, basi wangegundua kuwa mimi ndiye msanii pekee wa Taarab kwa sasa ambaye ninajaza kwenye shoo zangu, sasa sijui wanataka nirudi vipi mjini?” Anahoji Mzee Yusuf ambaye awali alitangaza kuacha muziki na kumtumikia Allah, lakini akarevjea tena

 

Leave A Reply