The House of Favourite Newspapers

Mzee Yusuf Kufanya Balaa la Kwanza Dar Live Leo

0

MFALME wa Muziki wa Taarab, Mzee Yusuf, anatarajiwa kuunguruma leo Agosti 7, mwaka huu, pale kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Mikito NusunusuMzee Yusuf amesema siku hiyo ndiyo mashabiki wake watajua alikuwa anamaanisha nini aliposema anarudi mjini.

 

Amesema amepokea maoni mengi kutoka kwa wadau tofauti na siku hiyo ataweka kila kitu wazi kuhusu uamuzi wake wa kurudi mjini na atashusha shoo baab’kubwa.

 

“Naomba mashabiki wangu wafike kwa wingi, kama mnavyojua huwa sinaga kazi mbovu mjini, mfalme narudi tena narudi kwa kishindo kikubwa, nimejipanga kuwapa burudani ya kutosha,” alisema Mzee Yusuf.

 

Kwa upande wake mratibu wa shoo hiyo, Rajab Mteta ’KP’,  amesema shoo hiyo ilikuwa ifanyike Julai 31 mwaka huu, lakini kutokana na msiba mzito uliolikumba taifa wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, ilisogezwa mbele.

 

“Niwaombe mashabiki wote wa Mzee Yusuf tukutane pale Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live Agosti 7 mwaka huu, Mzee anarudi mjini na ameahidi kufanya mambo ambayo hamjawahi kuyaona tangu ameanza kufanya muziki hadi pale alipoacha,” alisema KP.

 

Kabla ya kuacha kuimba Taarab, alikuwa tishio kwenye muziki huo ambapo ngoma zake kama Kaning’ang’ania, Mahaba Niue, Mpenzi Chocolate na Najiamini,  bado zinatamba mtaani mpaka sasa.

 

STORI: Mwandishi Wetu

 

Leave A Reply