The House of Favourite Newspapers

Mzee Yusuf, Vee Money kufunika leo Dar Live

0

MZEE-YUSUPHMfalme wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf.

MWANDISHI WETU, RISASI
ILE Ngoma ya Mashallah iliyoimbwa na Mfalme wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf kwa kushirikiana na staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee inatarajiwa kufunika leo (Jumamosi) kwa mara ya kwanza ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

mdeea-778x1024Vanessa Mdee

Akizungumza na Risasi Jumamosi mratibu wa shoo hiyo, Seif Magwallu ‘Shiboli’ alisema kuwa mbali na kupigwa ngoma hiyo ambayo ni habari ya mjini kwa sasa, mashabiki pia watapata fursa ya kulisikia kundi la muziki wa Taarab lisilo na mpinzani Bongo, Jahazi Modern likishusha kwa mara ya kwanza albamu mpya ya kundi hilo inayotambulika kama Kaning’ang’ania.
“Pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia saa mbili usiku hivyo mashabiki wa burudani waje kwa wingi kusikia kwa mara ya kwanza nyimbo zilizomo katika albamu hiyo mpya kama vile Hilo Limekuuma ya Fatma Ally, Nia Safi Hairogwi ya Mish Mohyamed, Nina Moyo Sina Jiwe ya Leila Rashid pamoja na Mashallah ya Mzee Yusuf akiwa na Vanessa Mdee,” alisema Shiboli na kuongeza kuwa Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa naye atakuwepo. Mratibu huyo aliongeza kuwa, kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 tu getini.

Leave A Reply