Mzee Yusuph Kufumbua Fumbo Dar Live

Baada ya Mfalme wa Taarabu hapa nchini, Mzee Yusufu kuja na Narudi Mjini, sasa aja kufumbua fumbo na shoo ya kukata na shoka pale Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Gazeti hili muandaaji wa shoo hiyo Rajab Mteta (KP) amesema, tarehe 25 mwezi huu pale Dar Live Mbagala, Mzee Yusuf atakuwa na jambo, lengo ikiwa ni kutambulisha bendi mpya na wasanii wake, ambayo imekuwa ni fumbo kwa mashabiki.

 

“Mashabiki wanaombwa kufika kwa wingi kwani Mzee anatarajia kufanya makubwa baada ya shoo ya kukata na shoka ya Narudi Mjini hii ya sasa itakuwa ni zaidi maana ataenda kutambulisha bendi yake mpya na wasanii jambo ambalo limekuwa ni fumbo kwa mashabiki wa taarabu.

 

“Kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000 tu na kutakuwa na wasanii kibao ambao watamsindikiza mfalme Mzee Yusuf, hivyo mashabiki wafike kwa wingi kwa ajili ya kupata burudani,’’ alisema KP.

 

Muda ni kuanzia saa mbili za usiku na mashabiki wanaombwa kuwahi mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha.

Stori: Happyness Masunga, Dar es Salaam
Toa comment