‘Mzimu’ wa Ajali ya Morogoro Waibukia Kenya

POLISI leo wameifunga barabara kati ya Nakuru na  Naivasha nchini Kenya katika eneo la Hoteli ya Stem huko Nakuru baada ya lori la mafuta lililokuwa linavuja, kumwaga mafuta hayo barabarani.

 

Akielezea hali hiyo, mkuu wa polisi (OCPD) wa Nakuru Mashariki, Ellena Kabukuru, amesema wameelekeza watumiaji wa barabara hiyo katika njia mbadala.

 

Vilevile, polisi wamewaonya wananchi kutojaribu kuyachota mafuta hayo ili kuepusha janga.

 

Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya ajali iliyoua watu zaidi ya 70 nchini Tanzania, mkoani Morogoro, kufuatia mlipuko wa moto uliotokea wakati watu wakichota mafuta hayo.


Loading...

Toa comment