The House of Favourite Newspapers

ads

Mzozo wa DRC: Matumaini Mapya Baada ya Mazungumzo ya Amani ya DR Congo Kuanza Nchini Kenya

0
Rais wa Kenya William Ruto (aliyekaa kushoto), Evariste Ndayishimiye wa Burundi (katikati) na rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia), pamoja na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika mziwa makuu Huang Xia (wa 3 kutoka kulia kwa waliosimama) Nairobi Kenya Nov 28 ,2022

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameelezea matumaini yake kuwa mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaweza kutatuliwa ikiwa michakato inayohusika itafikia sababu kuu ya mzozo huo.

Akizungumza kwa njia ya video wakati wa mazungumzo ya amani ya Nairobi yaliyoongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Kagame alihusisha mzozo huo wa miongo kadhaa na makubaliano ya awali ambayo hayakutekelezwa yaliyoanzishwa ili kuwezesha amani katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.

“Ninaamini kwa dhati kwamba juhudi hizi zitaleta matokeo mazuri.” Alisema Kagame.Mazungumzo yaliyoanza Jumatatu yataendelea hadi Jumamosi na yatahusisha jumuiya za mitaa, viongozi, mashirika ya kiraia na serikali.

Wanaunda uingiliaji wa tatu wa mchakato wa amani wa Nairobi kati ya Congo ambao pia uliwaleta pamoja wakuu wa nchi wanachama wa EAC, wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na wanadiplomasia kutoka nchi kadhaa.

Rais William Ruto aliyataja mazungumzo hayo kama kazi kuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki hadi mgogoro wa DRC utatuliwe.Bw Kenyatta alithibitisha kwamba makundi mengi yenye silaha yamepunguza uhasama tangu mazungumzo hayo yaanze, hivyo kuwezesha jamii zilizoathiriwa na vita kupata misaada ya kibinadamu, lakini akaonya kuwa wengine bado hawajafanya hivyo.

Alizitaka nchi wanachama wa EAC kuendelea kupeleka askari wao kufanya hivyo, kwa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa jumuiya hiyo.Burundi na Kenya zimetuma wanajeshi wao na Uganda inatarajiwa kupeleka wanajeshi wake katika wiki zijazo.Sudan Kusini imetuma maafisa wake wa wafanyakazi kabla ya kutumwa kwa wanajeshi wake katika mwezi ujao.

Rwanda na Uganda zilisema zinataka mzozo huo kutatuliwa ili kupunguza shinikizo la wakimbizi huku nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki zikitumai kumaliza mzozo huo ili kuruhusu biashara katika eneo hilo.

Rais Yoweri Museveni alisema Uganda iko tayari kutekeleza jukumu lake katika kumaliza mzozo huo na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa EAC kuchanganya juhudi ili jumuiya hiyo isikose nafasi nyingine ya kuleta amani ya kudumu Mashariki mwa Congo.

Hata hivyokundi la waasi la M23 siku ya Ijumaa lilikaidi wito wa kusitishwa kwa mapigano, likitaja mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa jeshi la Congo, FARDC, lakini wakaomba kukutana na mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Uhuru Kenyatta na Rais wa Angola Joao Lorenco, kutetea kesi yao.

Leave A Reply