Mzumbe University Yatangaza Nafasi 46 Za Ajira Kwa Wahadhiri
Chuo Kikuu cha Mzumbe kimetangaza nafasi 46 za ajira katika nafasi za kitaaluma (academic positions), kikialika Watanzania waliobobea na wenye sifa stahiki kuwasilisha maombi yao.
Kupitia tangazo rasmi lililotolewa na uongozi wa Chuo hicho, nafasi hizo zinapatikana katika kada mbalimbali za ualimu wa vyuo vikuu, zikiwemo nafasi za Wahadhiri Wasaidizi, Wahadhiri wa Kawaida, na nafasi nyingine ndani ya vitivo na idara mbalimbali za kitaaluma.
Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 6 Julai, 2025. Waombaji wote wanatakiwa kuzingatia sifa zilizotajwa kwenye tangazo rasmi na kuambatisha nyaraka muhimu kama vyeti vya elimu, wasifu binafsi (CV), na vielelezo vya uzoefu wa kazi.