Mzungu akiona cha moto

MZUNGU SEGEREA (1)
Akiwa chini ya ulinzi.

CHANDE ABDALLAH

SHERIA yachukuwa mkondo wake. Hilo limejidhihirisha baada ya Henry Domzalski (66), raia wa Marekani aliyedaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya bangi mwaka 2013 nyumbani kwake Msasani Beach jijini Dar kujikuta akihenyeshwa mahakamani na hatimaye kuhukumiwa miezi mitatu jela.

MZUNGU SEGEREA (2)Hukumu hiyo iliyosomwa Oktoba 29, mwaka huu mchana kweupe katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mbele ya hakimu Issa Kasailo na kuendeshwa na Wakili wa Serikali, Malangwe Mchungahela aliyesema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika hivyo mahakama hiyo itoe hukumu.

MZUNGU SEGEREA (3)Maofisa wa Polisi wakijadiliana jambo.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Kasailo alisema kuwa baada ya mahakama kupitia ushahidi na upande wa utetezi na kujiridhisha, imemtia hatiani Henry kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya bangi kiasi cha kilo 135.67 nyumbani kwake hivyo mahakama hiyo inamhukumu kutumikia miezi mitatu katika Gereza la Keko bila faini.

Hata hivyo wakili wa upande wa utetezi, Hudson Ndusyepo aliiomba mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwa kile alichodai kuwa hilo ni kosa la kwanza kwake pia ni raia wa kigeni ambapo hakimu huyo alisema kuwa rufaa ipo wazi kwa mtuhumiwa huyo kama hajaridhika na hukumu hiyo.

MZUNGU SEGEREA (4)Akipandishwa kwenye karandinga.

Akiwa mahakamani hapo, mwandishi wetu alishudia Henry akiwa amezungukwa na askari magereza na kasha kusindikizwa kwenda kukwea karandinga tayari kuanza kutumikia kifungo chake katika gereza la Keko.

Henry aliwahi kuwa mfanyakazi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Henry Domzalski (64) na kustaafu mwaka 2008.


Loading...

Toa comment