The House of Favourite Newspapers

Mzungu wa Diamond ‘Alizwa’ Simu

0

880A1920-1Prodyuza mahiri kutoka nchini Norway, Carl Hovind.

musa mateja
Yamemkuta! Prodyuza mahiri kutoka nchini Norway aliyekuja Bongo kwa lengo la kusaka vipaji na kuvitangaza kimataifa, Carl Hovind ambaye pia anafanya kazi kwenye studio ya mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzikati aliionja joto ya jiwe baada ya kuibiwa simu yake ya kisasa, iPhone 6s.

Mwenyewe anadai msala huo ulimpata akiwa ndani ya ukumbi wa burudani wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulikokuwa na shoo maalum iliyowakutanisha wasanii kibao pamoja na wadau wa muziki ambapo prodyuza huyo alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

“Tulikuwa tunafurahi na marafiki na kupiga stori za hapa na pale, kuja kushtukia simu yangu, iPhone 6s haipo. Hata sijui niliibiwaje maana muda wote ilikuwa mfukoni.

imeumia sana kwa sababu ina vitu vyangu kibao zikiwemo kazi zangu na mawasiliano ya nyumbani Norway na Marekani,” alisema Carl kwa masikitiko.

Leave A Reply