The House of Favourite Newspapers

Mzungu Wa Toto Abeba Vitanda Vyake

Toto Africans

MFADHILI wa Toto Africans ambaye ni raia wa Ujerumani, Jurgen Seitz ameamua kuchukua vitanda ambavyo alikabidhi kwa klabu hiyo kutokana na wahusika kushindwa kuvi­tunza.

 

Hii ni baada ya Toto kushuka daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza na sasa ipo Ligi Daraja la Pili.

 

Mzungu amefikia hatua hiyo ya kuchukua vitanda baada ya kudaiwa kuwa baadhi ya wanachama wa timu hiyo waligawana magodoro na ikaonekana kuwa utunzaji wa vifaa umekuwa mbovu.

 

Spoti Xtra lilimtafuta Kenneth Petro maarufu kama Dr Ken ambaye ni mwanachama wa Toto na mwakilishi wa mfadhili huyo akasema; “Nimeamua kuvi­chukua vitanda hivyo kwa ajili ya kuvitunza baada ya kuona havina usimamizi mzuri na nimefanya hivi kwa faida ya klabu kwani baadhi ya mali zingine zilipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Comments are closed.