The House of Favourite Newspapers

Nabi Aandaliwa Mkataba Mpya Yanga

0

TAARIFA za kuaminika kutoka ndani ya Yanga, zinadai kuwa viongozi wa timu hiyo wamepanga kumuongezea mkataba kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi.

 

Uamuzi huo umekuja baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo tangu Nabi apewe jukumu la kuinoa kutoka kwenye mikono ya Cedric Kaze, huku pia akitoka kuifunga Simba.

Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Viongozi wetu wa Yanga na wale wa GSM wameridhishwa na uwezo wa Nabi, ukiangalia amekaa muda mfupi tu lakini kuna mabadiliko makubwa sana yameonekana kwenye timu, hivyo wameanza kujadili suala la kumuongezea mkataba ili aijenge timu zaidi.

 

Spoti Xtra lilimtafuta Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro kuzungumzia hilo, alisema:

 

“Kiukweli Nabi alikuwa chaguo letu na ndiyo maana tulimpa kazi kwa sababu tulitambua ni mtu wa namna gani.“Kuhusu kuibadilisha Yanga ni kweli kafanya hivyo.

 

Lakini kuhusu mkataba mpya ni mapema sana kuzungumzia.”Nabi alitua Yanga April mwaka huu na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kwenye michezo sita ya ligi, ameshinda minne, sare moja na kupoteza moja.

Stori: SAID ALLY,Dar esSalaam

Leave A Reply