The House of Favourite Newspapers

Nabi Afichua Mazito Kipigo Cha Waarabu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa

0
Nasreddine Nabi.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amefunguka kuwa, sababu kubwa iliyopelekea kufanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Waarabu, US Monastir, ni kutokana na kupata muda wa kutosha kuwasoma wapinzani wake hao.

Nabi ametoa kauli hiyo kufuatia Yanga kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir ya Tunisia katika mchezo uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Yanga imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ikiwa imefikisha pointi kumi sawa na US Monastir, bado ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya TP Mazembe wa kukamilisha ratiba ya Kundi D.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema: “Kitu cha kwanza kikubwa upande wetu kwa sasa tumeweza kufikia malengo ya kufuzu hatua robo fainali kwa sababu ndiyo ilikuwa dhamira kubwa kwetu ingawa tulitambua ugumu ambao tunaweza kukutana nao.

“Nadhani maandalizi yetu pamoja na muda wa kutosha tulioupata katika kuwasoma wapinzani kutokana na makosa ambayo yalijitokeza mchezo uliopita yamepelekea kwetu kujipanga na kupata ushindi ingawa bado tunahitaji kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho kule Lubumbashi.”

STORI NA IBRAHIM MUSSA

Leave A Reply