Nabi Aomba Mashine Tano Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi amekabidhi ripoti ya usajili iliyopendekeza kusajili
wachezaji watano pekee.


Hiyo ni katika kuelekea usajili wa dirisha dogo ambao dirisha lake lililofunguliwa Desemba 15, mwaka huu.


Yanga tayari imemalizana na kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakari atakayejiunga na timu hiyo muda wowote kuanzia sasa. Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Jumatatu kuwa wachezaji hao watano anaowataka Nabi, watatu ni wazawa na wawili ni wakigeni.


Bosi huyo alisema kuwa wach-ezaji hao wa kigeni wote ni viungo washam-buliaji wa pembeni.
Aliongeza kuwa wachezaji wa kigeni wote hao watatokea nchini DR Congo.


“Hatutaki masihara katika msimu huu hatutasajili straika tena wa kati kutoka nje ya nchi na badala yake tutasajili viungo wawili washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.


“ Pia tutasajili wazawa watatu kati ya hao yupokiungo mchezaji ambaye ni Sure Boy ambaye tumamalizana naye tayari.


“Katika kukiimarisha kikosi chetu pia tutasajili mshambuliaji mmoja msumbufu wa kati mwenye
uwezo mkubwa wa kufunga mabao.


“ Usajili huo wote kwa asilimia kubwa ushakamilika kilichobakia wachezaji hao kusaini mkataba pekee,” alisema
bosi huyo.


Akizungumzia hilo Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, Injinia Hersi Said alisema kuwa “Tumepanga kufanya usajili wa kishindo katika usajili huu wa dirisha dogo kwa kufuata ripoti ya usajili wa kocha wetu.

STORI NA WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA704
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment