The House of Favourite Newspapers

Nabi Apata Majembe ya Kazi Yanga

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, leo anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wake wa tano mbele ya Mwadui FC baada ya kurithi mikoba ya mtangulizi wake Cedric Kaze.

 

Akielekea kwenye mchezo huo wa leo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, tayari ameshapata majembe yake manne ya kazi kwa upande wa ulinzi.

 

Nabi raia wa Tunisia, amekiongoza kikosi hicho katika mechi nne ambapo alishinda mbili, sare moja na kupoteza moja ndani ya dakika 360.

 

Kwa upande wa safu ya ulinzi anamuamini Metacha Mnata ambaye rekodi zinaonesha kwamba alikaa langoni kwenye mechi tatu, alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC.Kibwana Shomary na Adeyum Saleh, wote wamecheza mechi zote nne.

 

Kwa upande wa Dickosn Job, amecheza mechi tatu na hakuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Prisons wa Kombe la Shirikisho.

Mbali na nyota hao wanne ambao ni chaguo lake la kwanza, pia yupo Bakari Mwamnyeto na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao kwenye mechi nne walianza kikosi cha kwanza katika mechi mbili, huku Shaibu akikosekana kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na JKT Tanzania kwa kuwa ni mejeruhi.

 

Nahodha Lamine Moro alianza kikosi cha kwanza mchezo mmoja, ulikuwa wa Kombe la Shirikisho mbele ya Tanzania Prisons, ila kwa sasa amepigwa pini kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu.

 

Mechi zake ilikuwa ni Aprili 25 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-1 Azam FC.

 

Kombe la Shirikisho, Aprili 30 hatua ya 16, Tanzania Prisons 0-1 Yanga. Mei 15, Namungo 0-0 Yanga na Mei 19, JKT Tanzania 0-2 Yanga.Nabi aliliambia Spoti Xtra kuwa, kila mchezaji ana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na juhudi ambazo atazionesha katika mazoezi.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar

Leave A Reply