The House of Favourite Newspapers

Nabi Ashusha Majembe Nane ya Maana

0

JUMLA ya majina nane wamekabidhiwa Kamati ya Mashindano ya Yanga iliyo chini ya Makamu Mwenyekiti, Injinia Hersi Said, ili kushusha majembe ya maana kuelekea msimu ujao.

 

Kocha Mkuu wa timu hiyo raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, ndiye aliyekabidhi majina hayo katika kamati hiyo tayari kufanya usajili.Mmoja wa mabosi wakubwa ndani ya Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, kocha huyo hadi hivi sasa amependekeza kufanyika maboresho ya haraka ya kikosi kwa kusajili katika maeneo matatu baada ya kukaa na kikosi hicho kwa zaidi ya mwezi mmoja.

 

Bosi huyo aliyataja maeneo hayo ni kipa, mabeki wawili wa pembeni na kati, kiungo na ushambuliaji ambalo ndiyo eneo la kwanza walilopania kulirekebisha kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na uzoefu.Aliongeza kuwa, upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kuwatema baadhi ya wachezaji wake sita wa kigeni na kubaki na wanne katika msimu ujao kwa ajili ya kuachia nafasi ya kuwasajili wengine.

 

“Kocha tayari amependekeza usajili wa wachezaji nane katika kukiimarisha kikosi chetu ambacho msimu ujao kitashiriki mashindano ya kimataifa.

 

“Kati ya wachezaji hao tutakaowasajili yupo kipa, kiungo, washambuliaji, beki wa kati na pembeni wawili, tayari tumemsajili mmoja ambaye ni Djuma Shaban, hivyo bado mwingine mmoja.“Wachezaji hao wote wamependekezwa na kocha Nabi, kati ya hao wapo wa kigeni na wazawa ambao amewaona katika michezo ya ligi na Kombe la FA.

 

“Hivyo kama uongozi tumepanga kuwasajili wachezaji wote waliokuwepo katika mipango ikiwemo kuvunja mikataba kwa wale waliokuwa nao katika klabu zao,” alisema bosi huyo.Hassani Bumbuli ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Usajili wetu tunaufanya kwa siri kubwa sana, hivyo muda ukifika mtaona mambo.”WILBERT MOLANDI, Da

Leave A Reply