The House of Favourite Newspapers

Nabi Ashusha Presha Yanga, Atoa Kauli ya Kibabe

0

KOCHA Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa watarajie furaha katika michezo ijayo kutokana na maboresho makubwa anayoendelea kuyafanya Hiyo ni baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara walipocheza dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

 

Timu hiyo hivi sasa ipo katika maandalizi ya mchezo wa Kombe la FA watakaocheza Jumanne ijayo dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Akizungumza na Championi Jumamosi, kwa niaba ya Nabi kocha wa makipa wa timu hiyo, Razack Siwa alisema kuwa kadiri ya siku zinavyokwenda anaona mabadiliko ya kikosi chake kutokana na kucheza kwa kufuata maelekezo anayowapa mazoezini.

 

Siwa alisema kuwa bado anaendelea kuyafanyia baadhi ya maboresho ikiwemo safu ya ushambuliaji. Aliongeza kuwa ana matumaini makubwa ya timu yake kupata matokeo mazuri sambamba na vijana wake kucheza soka safi la kuvutia kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki.

 

“Kikubwa mashabiki wanatakiwa kuwa na subira kwani bado kocha ni mpya, hivyo ana sera yake ya aina ya uchezaji.

“Hakuna kitakachoshindikana, hivi sasa wanaziboresha baadhi ya nafasi ikiwemo ya ushambuliaji, hivyo mashabiki waondoe hofu wajiandae kupata furaha katika michezo ijayo ya ligi ya Kombe la FA.

 

“Mabadiliko yameanza kuonekana katika michezo iliyopita ukiwemo dhidi ya JKT Tanzania, kila shabiki ninaamini alifurahia kuona vijana wakipambana huku wakicheza soka safi la kuvutia,” alisema Siwa.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply