Nabii Bushiri mahakamani kwa kutakatisha fedha

NABII wa aina yake asiyeishiwa vituko, Shepherd Bushiri, amefikishwa mahakamani jijini Johannesburg leo ambako yeye na mkewe wanakabiliwa na mashtaka ya kutakatisha fedha.  Hii si mara ya kwanza kwa mtu huyo kufikishwa mahakamani kwa makosa yanayohusiana na fedha.

Mwaka jana, alitiwa mbaroni kwa kusafirisha mamilioni ya fedha (rand) kutoka Afrika Kusini kwenda Malawi.  Pia aliingia matatani mwezi Desemba mwaka jana baada ya kutokea ghasia kwenye kanisa lake ambapo waumini watatu walifariki.

 

Loading...

Toa comment