NABII DKT. LUCY NATASHA AKONGA MAMIA WALIOJITOKEZA MKUTANO WA INJILI

Nabii Dkt.  Lucy Natasha akiingia katika Uwanja wa Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa neno la kinabii kwa mamia huku akishangiliwa kuonesha wako tayari kupokea upako na miujiza toka kwa bwana.

Mamia ya watu waliojitokeza kwenye mkutano huo wakipokea upako.

…Dkt.Natasha akiombea mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Dkt. Lucy Natasha akiendelea na maombi.

NABII wa Kimataifa kutoka nchini Kenya, Dkt. Lucy Natasha amekonga mamia ya watu waliojitokeza katika  mkutano wa nje uliokuwa wa  kumsifu Mungu na maombezi.

 

 

Dkt.  Natasha akiingia katika Uwanja wa Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa neno la kinabii kwa mamia ya watu  hao, alilakiwa na kumshangiliwa kuonesha walikuwa tayari kupokea upako na miujiza toka kwa bwana.

 

Baada ya maombi hayo nabii huyo alimtabiria mtoto aliyepata uponyaji kuwa nabii wa mungu katika maisha yake hapo baadaye.

 

Mtoto huyu ni miongoni mwa watu waliopokea uponyaji toka kwa bwana ambapo kitovu chake kilichokuwa kikubwa tangu kuzaliwa kwake, lakini kupitia maombi haya mtoto huyo alipokea uponyaji kwa kurejeshewa kitovu chake katika hali ya kawaida.

 

Mbali na mototo huyo pia mwanaume mwingine ambaye aliteseka na tatizo la macho kwa muda wa miaka 29 naye hii leo alipokea uponyaji na kuweza kuona kupitia nabii huyo.

 

 

Leo ni siku ya tano katika mkutano huo unaoendelea viwanjani hapo na unatarajiwa kumalizika Julai 07 mwaka huu na  uliandaliwa na kanisa la RGC kwa mtumishi wa mungu Nabii Dkt. Peter Nyaga ambapo kupitia muhubiri wa kimataifa Nabii Dkt.Lucy Natasha, mungu ametenda miujiza ya ajabu ikiwemo kumponya mtoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja ambaye alikuwa hawezi kutembea.

 

Loading...

Toa comment